Ad Code

Responsive Advertisement

Unaweza Kutuma Meseji Normal Kwa Mtu Hata Kama Huna SMS Kwenye Laini Yako?


Je wajua kuwa unaweza kutuma meseji normal kwa mtu hata kama huna SMS kwenye laini yako? Kikubwa uwe na MBs au WiFi connected🥷 Yaani unachat Normal na mtu kwa kutumia MBs na inakuwa mfumo kama WhatsApp tu delevered, seen, typing na zaidi👊.

Katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia, mawasiliano ni muhimu sana. Ingawa wengi wetu tunategemea SMS za kawaida, kuna njia bora zaidi ya kuchat kwa kutumia data au WiFi bila kuwa na SMS kwenye laini yako. Mfumo huu unaitwa RCS Chats, na unapatikana kwenye app ya Google Messages. Kupitia makala hii, tutakufundisha jinsi ya kuwezesha RCS Chats na kufurahia mawasiliano ya hali ya juu kama kwenye WhatsApp, ikiwa na huduma kama delivered, seen, na typing. Karibu ujifunze zaidi na kuboresha uzoefu wako wa kuchat!

Cha kuzingatia: Lazima na yeye awe amewasha data sasa huu mfumo unaitwa RCS Chats, Unapatikana kwenye app ya Google SMS/ Google Message.

Utaingia Setting then Message Setting halafu RCS Chat weka ON, Halafu Connect na namba yoyote ya laini yako kisha washa data na anza kuchat kwa kutumia MBs pale ambapo unaechat nae atakuwepo ONLINE pia.

Ili ujue kuwa yupo online au amewasha data na app yake ya SMS inasupport RCS Chat ukiwa unasend text itajiconnect automatically kwenda mfumo wa RCS chat na atapokea na utaweza kuona Delivery Report na Read Receipt na hata akiwa anatype utaona pia🥷.

Faida za RCS Chats.
Delivered, Seen, Typing, Kama WhatsApp, utaweza kuona meseji ikiwa imefika, imesomwa, na kama mtu anaandika.
Delivery Report na Read Receipt, Utaweza kuona ripoti ya kufika na kusomwa kwa meseji.
Device Pairing, Unaweza kupair na kifaa kingine ili kuona meseji zako.

Tahadhari.
Mtu Anayechati Naye Lazima Awe na Data, Ili mfumo huu ufanye kazi, lazima mtu unayechati naye awe amewasha data na app yake ya SMS inasupport RCS Chat.
Usalama, Hii app inaweza kusaidia kuhack texts za mtu kama utafanikiwa kushika simu yake na akawa anatumia app kama hii kwa kutap sehemu ya Device Pairing na kupair simu yake.

Kwa kumalizia, RCS Chats inabadilisha jinsi tunavyowasiliana kwa SMS za kawaida kwa kutoa huduma za kisasa zinazopatikana kwenye majukwaa ya kuchat kama WhatsApp. Kwa kufuata hatua zilizoelezwa kwenye makala hii, utaweza kuwezesha RCS Chats kwenye Google Messages na kufurahia mawasiliano bora zaidi. Uwezo wa kuona meseji zikiwa delivered, seen, na typing hufanya mawasiliano yako yawe ya haraka na yenye ufanisi. Jaribu sasa na uone jinsi RCS Chats itakavyobadilisha uzoefu wako wa kuchat!



Post a Comment

0 Comments